SHIUMA WAANZA KUSAJILI WANACHAMA KWENYE KANZI DATA - KILIMANJARO

Pichani ni uongozi na wanachama wa SHIUMA Kilimanjaro katika moja ya vikao vya halmashauri, tukio lililojumuisha uzinduzi wa mradi wa kusajili wanachama kwenye kanzi data ya shirika. 

Willy Kavishe anaripoti, " Leo tarehe 31/10/2023 tumefanya uzinduzi wa kusajili wafanya biashara ndogo ndogo (machinga) mkoani Kilimanjaro, mgeni rasmi akiwa ni mkuu wa mkoa pamoja na wakuu wa wilaya zote. Tumeanza kusajili viongozi wa SHIUMA mkoa sambamba na ugawaji wa vocha kwa viongozi wa SHIUMA ngazi za wilaya zote."

Advertisement produced on behalf of Tiva Insurance Tanzania LTD and seeking to obtain business for insurance underwritten by Tiva Insurance is underwritten by

top-arrow